Exodus 27:10-15

10pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 11Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

12“Upande wa magharibi wa ua utakuwa na upana wa dhiraa hamsini,
Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.
nao utakuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi.
13Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, ua pia utakuwa na upana wa dhiraa hamsini. 14Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 15Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tano
Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75.
kwa upande mwingine wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu.

Copyright information for SwhKC